Posts

Showing posts from April, 2023

196 - Vito Vya Thamani

  196 - Vito Vya Thamani     "When He Cometh" 1. Kitambo Bwana yuaja, atafute kote  Vito vya thamani kubwa: mali yake kuu. Kama nyota tajini vitang`aa sana,  Vito vizuri kweli vyenye thamani. 2. Karibu atakusanya vito kwa ufalme,  Vizuri vinavyong`aa: mali yake kuu. 3. Watoto wote wadogo wampendao Yesu,  Ndiyo vito ving,vyo: mali yake kuu. (Amina)

197 - Anipenda Ni Kweli

  197 - Anipenda Ni Kweli     "Jesus Loves Me" 1. Anipenda ni kweli: Mungu anena hili;  Sisi wake watoto kutulinda si zito. Yesu Mwokozi ananipenda; Kweli hupenda, Mungu  amesema. 2. Kwa kupenda akafa niokoke na kufa:  Atazisafi taka sana ataniweka. 3. Anipenda kabisa; niuguapo sasa,  Anitunza mbinguni niliyelala chini. 4. Kunipenda haachi tu sote hapa chini,  Baada ya mashaka kwake tanipeleka   (Amina)

198 - Kaza Sana Macho

198 - Kaza Sana Macho "I Washed My Hands" 1. Nilinawa mikono safi asubuhi, Itende kazi kutwa kwa Yesu, Yesu Mwokozi. Kaza sana macho njiani kote, Utende kwa Yesu kazi njema tu. 2. Natega masikio nitambue wasaa, Mikono na itende upole daima. 3. Macho yangu yachunga mikono kazini; Ilindwe maovuni impendeze Yesu.    (Amina)

199 - Upendo Ni Furaha

199 - Upendo Ni Furaha 1. Upendo ni furaha, ni kweli desturi; Yake kuzisahihisha, njia zetu zote. Yu pendo: tu watoto wake, Yu pendo, Mwana wa Mungu! 2. Na sisi tupendane  kama Baba Mungu, Amri yake ndiyo hii, kupendana sana. 3. Duniani huzuni, ugonjwa mauti; Kwa pendo tuwafariji, wenye mahitaji. 4. Na atakapokuja kutuchukua juu; Tutaimba milele pendo lake Yesu.   (Amina)

200 - Baba Yetu Aliye Mbunguni

  200 - Baba Yetu Aliye Mbunguni "I Am So Glad That Our Father In Heaven" 1. Baba yetu aliye mbinguni, Amenifurahisha yakini. Kuniaambia mwake Chuoni, Ya kuwa name Yesu pendoni. Anipenda Mwokozi Yesu, Anipenda, Anipenda;  Anipenda Mwokozi Yesu, Anipenda mimi. 2. Nimuachapo kutanga mbali, Yeye yu vivyo, hupenda kweli: Hunirejea kwake moyoni, Kweli yu name Yesu pendoni. 3. Anipenda! Nami ninampenda, Kwa wokovu alionitenda; Alinifilia msalabani, Kwa kuwa name Yesu pendoni. (Amina)

201 - Hunipenda Pia

 201 - Hunipenda Pia  "He Loves Me Too" 1. Mungu huona videge wanaoanguka; Akiwapenda videge, vile hunipenda. Hunipenda, hunipenda, hunipenda pia; Najua ananipenda niliye mdogo. 2. Rangi ya namna nzuri hupamba maua; Akiyapenda maua, vile hunipenda. 3. Mungu aliyeviumba videge, maua, Hatasahau watoto, kweli huwapenda.   (Amina)

202 - Sikia Mlio

202 - Sikia Mlio "Hear The Pennies Dropping" 1. Sikia mlio! Pesa koponi  Zinalialia - zote kwa Yesu. Kuanguka kuanguka pesa koponi, Kila moja kwako, Yesu zipokee. 2. Huanguka pesa toka mikono:  Sadaka kwa Yesu ya kundi dogo. 3. Tulio wadogo tuna haba tu;  Tuishapo kua pendo `tazidi. 4. Wenye mali chache tumpe moyo;  Kwa furaha tupu atakubali   (Amina)

203 - Ya Saba Ni Kwa Yesu

 203 - Ya Saba Ni Kwa Yesu " The Seventh Is For The Lord" 1. Siku sita fanya kazi, Ya saba ni kwa Yesu.  Hapo tunapopumzika, kwani ni yake Yesu. Moja, mbili, tatu, nne, tano, sita, zote kwetu;  Lakini tutakumbuka, Ya saba ni kwa Yesu! 2. Huonyesha ya kufanya, Kwa kuwa ni ya Yesu,  Na atuonyesha njia, tutamfuata Yesu. 3. Tuombe kila Sabato, Na kujifunza kwake;  Tutamtii daima, tutakaa na Yesu (Amina)

204 - Kuwa Na Yesu Nyumbani

  204 - Kuwa Na Yesu Nyumbani     "Happy, Happy Home" 1. Kuwa na Yesu nyumbani, Furaha nyingi,  Furaha nyingi, furaha nyingi.  Kuwa na Yesu nyumbani.  Furaha nyingi, furaha nyingi. 2. Yesu yu ndani ya Baba, Nyumba salama,  Nyumba salama, nyumba salama;  Yesu yu ndani ya Baba.  Nyumba salama, nyumba salama. 3. Yesu yu ndani ya Mama, Nyumba salama,  Nyumba salama, nyumba salama;  Yesu yu ndani ya Mama.  Nyumba salama, nyumba salama 4. Yesu ndani ya watoto, Nyumba salama,  Nyumba salama, nyumba salama;  Yesu yu ndani ya watoto.  Nyumba salama, nyumba salama. (Amina)

205 - Msifu Mungu Ee Watoto

205 - Msifu Mungu Ee Watoto   "Praise Him! Praise Him! 1. Msifu Mungu, Ee watoto wote, Yu pendo, Yu pendo;  Msifu, Msifu, Ee watoto wote Mungu ni upendo. 2. Tunampenda, Ee watoto wote, Yu pendo, Yu pendo,  Tunampenda, Ee watoto wote Mungu ni upendo. 3. Tumikeni, Ee watoto wote. Yu pendo, Yu pendo,  Tumikeni, Ee watoto wote Mungu ni upendo.    (Amina)

206 - Mwokozi Wangu Anipenda

 206 - Mwokozi Wangu Anipenda "Now I Belong To Jesus" 1. Mwokozi wangu alinipenda,  Maovu ayanitengi naye,  Alijitoa, kuniponya,  Sasa mimi wake.  Mimi wake kabisa,  Naye Yesu wangu,  Si kwa wakati huu tu,  Bali na milele.  2. Dhambi nilijidhili sana,  Yesu akaja kunikomboa,  Akanitoa sumbukoni,  Sasa mimi wake.  3. Furaha nyingi moyoni mwangu,  Bwana Yesu kunifanya huru,  Kunitwaa kwa damu yake,  Sasa mimi wake. (Amina)

207 - Nani Afanya Maua

207 - Nani Afanya Maua "Who Makes The Flowers" 1. Nani ayafanya maua, maua,  Nani ayafanya, Mungu juu.  2. Nani apambaye machweo, machweo,  Nani ayapamba, Ni Mungu.  3. Nani afanya theluji, theluji,  Nani aifanya, ni Mungu.  (Amina)

208 - Mungu Afanya Upinde

 208 - Mungu Afanya Upinde "The Rainbow" 1 . Nani afanya upindi,  Namjua, namjua  Mungu afanya upindi  Nampenda kwa hiyo.  2. Mungu atuma upindi  Ni bora mweupe,  Mungu atuma upindi,  Kwamba yu karibu. (Amina)

209 - Nakupenda Sana Kufika

 209 - Nakupenda Sana Kufika "I Love To Come To Sabbath School" 1. Napenda sana kufika, skuli ya Sabato  Napenda sana kufika, skuli ya Sabato 2. Napenda sana kuimba, habari za Yesu,  Napenda sana kuimba, siku ya Sabato 3. Napenda sana kutoa, sadaka kwa Yesu,  Napenda sana kutoa, siku ya Sabato 4. Napenda sana kuomba, kwa Yesu, kwa Yesu,  Napenda sana kuomba, siku ya Sabato 5. Napenda sana kujua, maneno ya Yesu,  Napenda sana kujua, siku ya Sabato 6. Napenda sana kusema, Fungu la kariri,  Napenda sana kusema, siku ya Sabato (Amina)

210 - Roho Wa Mungu Wangu

 210 - Roho Wa Mungu Wangu "Spirit Of The Living God" 1. Roho wa Mungu wangu, Nakuhitaji!  Roho wa Mungu wangu, Nakuhitaji!  Unilinde na unijaze;  Roho wa Mungu wangu, Nakuhitaji! (Amina)

211 - Moyoni

 211 - Moyoni "Into My Heart" 1. Moyoni, moyoni; Ingia moyoni, Yesu.  Njoo leo, njoo kukaa, Ingia moyoni Bwana.  Moyoni, moyoni, Angaza moyoni Yesu,  Ng'aa leo siku zote, Angaza moyoni Bwana. (Amina)

212. Mtazame Mwokozi

 212 - Mtazame Mwokozi "Turn Your Eyes Uppon Jesus" 1. Mtazame Mwokozi,  Usoni Mwake mzuri,  Mambo ya dunia hugeuka,  Usowake tukiuona. (Amina)

213. Niwe Nao Uzuri Wa Mwokozi

 213 - Niwe Nao Uzuri Wa Mwokozi 1. Niwe nao uzuri wa Mwokozi,  Nazo huruma Zake na usafi,  Roho Mtakatifu anibadilishe,  Aonekane Yesu ndani yangu. (Amen)

214. Nataka Niwe Tayari

 214 - Nataka Niwe Tayari 1. Nataka niwe tayari, Bwana,  Nataka niwe tayari, Bwana,  Furaha za ulimwengu ni bure; Nilinde hata uje! (Amen)

215. - Ulimwengu Wataka

 215. Ulimwengu Wataka 1. Ulimwengu wataka kumwona Yesu;  Ulimwengu wataka kumwona Yesu.  Analeta furaha, shangilio kutosha,  Ulimwengu wataka kumwona Yesu. (Amina)

216. - Moyoni Nijaze

 216 - Moyoni Nijaze 1. Moyoni 'nijaze,  Na Roho wa Yesu;  Nataka kujitoa,  Moyoni 'nijaze. "With Thy Spirit Fill Me" 2. Moyoni 'nijaze,  Na Roho wa Yesu;  Nataka kujitoa,  Moyoni 'nijaze. (Amen)

217. Omba Sana Asubuhi

 217 - Omba Sana Asubuhi 1 Omba sana asubuhi,  Omba sana mchana,  Omba sana na jioni,  Bwana hutusikia.  2 Mungu hujibu maombi,  Asubuhi na mchana,  Hata hutungojea tena,  Wakati wa jioni.  3 Na tuimbe asubuhi.  Tena saa za mchana.  Hivi tutafurahi Naye.  Pumziko la jioni. (Amen)

218. Yesu Mwokozi Mpendwa

 Yesu Mwokozi Mpendwa 1.  Yesu Mwokozi Mpendwa.  Hakuna mwingine!  Yesu Mwokozi Mpendwa,  Yesu Mwokozi Mpendwa,  Nakutazama wewe pekee,  Yesu Mwokozi Mpendwa,  Ninakutafuta;  Wewe u mali yangu.  Sasa na mileleaa (Amen)

219. Pambazuka Nuru

 219 - Pambazuka Nuru 1. Pambazuka nuru,  Siku mpya yaja,  Basi amkeni na kuimba,  Ninyi nyote!  Pambazuka nuru,  Siku mpya yaja,  Yesu atakaporudi kama Mfalme! (Amen)

220. Kwa Heri

 220 - Kwa Heri     1 Kwa heri, Mungu awalinde;  Kwa heri, na awaongoze;  Kwa heri, na kuwapa amani,  Bwana awabariki. (Amen)